1
Thessalonians 4:3 - For this is the will of God, [even]
your sanctification, that ye should abstain from fornication:
Shoga wa mie, mdogo wangu kwa
mwaka mmoja, aliuishi huu mstari karibia maisha yake yote ya utoto. Enzi hizo
tukiambiw mchumbaa, unaliaaa. Kila mtu mie sista. Loooh! Basi mtaani sie ndo
waimba kwaya. Utaamini Lara 1 mie, nilikuwa mtoto wa kipapa enzi hizo ndo
inaanza uniform za njano bado? Mpiga chakacha kanisani naimba sauti ya 1, na
dada wa mie sauti ya , maza hataki matani. Shoga angu nae mpiga ngoma kanisani,
na nguo zetu ndefu utatujuaaaa?
Kiukweli kilichotufanya tuimbe
kwaya sio upako wala nini, kwanza kanisa ilikuwa kigango cha mafather wahindi,
na masister wahindi, so chocolate za kumwaga. Wale watu wazima wenzangu wa mid
and late 1990s mtasema hapa mambo yalivokuwa adimu ya chocolate. Afu pili
watoto wa kishua wa Internationa l school walikuwa wanasali pale, wazungu, na
mitoto ya kibosi mingine. Nimesema International Schoo sio English Medium.
International School zipo 4 tu Bongo nzimaa mpaka na leo. 3 kulikuwa na
Seminary, kulikuwa na wakaka wazuri ni kiamaaaaaa. Looo, looo, looo. Acheni tu.
4. Kukwepa kwenda tution, afu church kuna distance so it was fun kwenda coz
mnaendesha baiskeli zenu, mnacheza njia nzima, and the beauty of it all
hamuendi tution. Usipoenda church, maza hataki masihara tution. 5 kushindana
mavazi ndo ilikuwa raha yetu. Kiukweli dada wa ie ndo alikuwaga anashinda kila
siku. Mos of our primary std 4,5,6 tumeimba kwaya sanaaa. Enzi hizo it was
cool! Na shoga wamie J ndo tulikulia mazingira hayo, ya alatareni. Watoto wa
bwana.
Kuna watu walianza anza kidogo
kuandikiana vibarua na waseminary si mnajua tena balehe za wengine zinawahi,
lakini mimi na J mdada wa maadili tulishika huo mstari mpaka mwishooooo.
Tukifika mazoezi mimi nachaka langu, yeye anapiga drums, wengine wanaimba.
Jumapili performance ya kufa mtu. Bi mkubwa anawahi mbele, akitoka anamwambia
kila mtu wanangu hawa! So proud of us! Hapo katununulia migauni chini ya
magoti. Sema nilichompendea baada ya mambo ya kwaya kunoga mambo ya wardrobe
akayaboresha, hakuna kurudia nguo jpili walau miezi 3. Alikuwa makiniii, kufatilia
nywele, viatu,magauni kama tupo smart. Hata yeye asipoenda church anatutimuaaa.
Utasikia yule mpiga chakacha mwingine ananiumiza masikio, twendeni mabinti
zangu mkanipigie instrumental za maana. Akawa anaifosi nijifunze na Piano,
chakacha is too local, too not stylish. Binti mpiga piano would have been a
plus. Bwana weee, babu wa piano alinifundisha weeee akaona sina kipaji, bi
mkubwa kapush weee wapiii. Ndo nikabakia mpiga chakacha. Hata mkinicheka nacho
kipaji mjue.
Hakukuwa na major event mpaka mi nilivofika
STD 6, maza akaniambia hela ya STD 7, sinaa. Fanya manuvaa ufanye mtihani wa
form 1, uanze. Englishmedium ghali sanaa. Kipanga wangu usiniangushe. Kweli
nikaenda form 1. Nikamuacha shosti J anapiga drums church. Chakacha akaanza
kupiga mtu mwengine. Nilivorudi nikawa sina interest tenaa na kwaya. Hapo dada
wa mie yupo form 2, ashaacha kwaya, ananiambia dogo kwaya ushambaaa. Ukipiga
chakacha mie kanisani siji wala nini. Anakunywaje bia sasa. Na mie namfata tu
nyuma nyuma. Ananiambia haya ndo maishaaa. Na wapagani wengine home pale ikawa
kanisani anaenda mdingi peke yake. Sasa wote watu wa kusafiri sanaa. Tukawa
tunajilea wenyew. Na cousin wangu akaw kaja kuishi pale kashindikana kwao, ndo
kaletwa kwa mjomba wake amnyooshe. Looooh! Tunajinywea bia tu, mama ake anampa
mihela kibaooo. Ndo kunywaaa, analeta mademu manake yeye alikuwa A level, party
kila siku. Mtaani watu wakawa wametuchokaaa. Wanawambia watoto zao msiende
nyumba ile kabisaaa. Wahuni wale wanaongeza na chumvi hapo. Hapo maza hayupo
anasoma zake huko micheti familia kaitelekeza.
J akawa anakuja kunishauri nirudi
kupiga chakacha church, nakubaliana nae, ila akiondoka dada wa mie ananiambia
achana na yule mpiga ngoma atakupotezaaa. All the cool boys cant hang with us
kama unapiga chakacha. Namuharibia. Atanitenga. Na yule mtu mzima hovyo
anamuunga mkono wamba hata kama party home wtakuwa hawanialiki. Ananipamba niwe
socialite wa mtaa. Basi Jpili J akinipitia siendi. Father mlezi akaiuliza mbona
huji kwaya, kanisani sionekani, nikawa nadanganya tu. Mwisho akapata file letu
ikawa akituona hatusalimii,na anatutolea mfano watu waepuke kuwa kama sisi. J
nae akakata tamaaa. Mwaka unaofata akaenda form 1 nae. STD 7 yote alikuwa
anasoma masomo pale mbele. Uzuri akaenda shule ya masista.
Romans
1:24-32 - Wherefore God also gave them up to uncleanness through the
lusts of their own hearts, to dishonour their own bodies between themselves.
Secondary siku interact na
J sanaa. Ila tukiwa me form 4, J form 3 alinipia simu, anataka tuongee kuna
ishu nyeti anataka kuniambia. Hapo bado anasoma masomo kanisani kama kawaida.
Mi nikamwambia sawa, nikajua anataka kunihubiria. Hapo church ndo siendi hata
miezi 6. Ndo nikawa nakaa hostel ndo kabisaa.
Tukakutana Mwenge, akaniambia
anaomba ushauri wangu, Kuna siku alimsindikiza shoga ake kumuona kaka yake
ambae ni brooder hapo seminary naitia kapuni ila hapa hapa jijini. Basi kufika
kule kw a mabrooder wakalaaaaa, wakafurahi, sasa akamkuta Fratery ambae nae
kaenda kutembea hapo kwa mabrooder ni Mzulu wa South huko. Hajui
Kiswahili fresh. Wakapiga story mbili tatu na nini, na shoga ake, na kaka mtu,
hivooo. Mda wa kuondoka wakiwa washaachana na kaka mtu, yule Fthaer
akawakimbilia akamuita yeye J peke yake.
Akamwambia nimependa kampani yako
mnooo. njoo Parokoia flani, niulizie Fratery flani, ila uje peke yako. Usije na
mtu. Mpo hapo wasomaji? Mmmmmmhhhhh! Akamgea na kikaratasi kina namba yake hio
ilikuwa 2005. Sasa akawa ananiomba ushauri aende asiende.
Mi nikaona hili sio swala la
kujiuliza anataka kwenda sema roho inmsuta. Roho ikawa inaniambia mshauri
asiende, ila nikakumbuka kwa mafather kuna Pizza, Pie, Mi cake, hatari sanaaa,
nikjikuta nimemshauri la msingi na mbolea tuongozane, asiende mwenyewe. Kiukweli
mi nilijua tu itaishia kwenye kula haiwezi kuwa kubwa kiasi hiko.
Kufika kama kawaida na sketi zetu
ndefu, tukamuulizia Fratery, maana namba ya simu haipatikani. Tukambiwa kaenda
South kumalizia utumishi wake. Mimi na domo langu kubwaaaa, nikauliza kwani ana
padrishwa lini? Nikaambiwa bado kuna kamda kidogo kakutumikia. Sasa yule Padri
akawa katu doubt ila anatumia saikolojia kutuchota akili tuseme yule mtumishi
watoo wa dogooo miaka 15 tunamtafutia nini? Afu sio mmbongo hatuwezi kuwa ndugu
zake. Sasa mi nikastukia ishu. Nikamdanganya mtumishi wa Mungu, alikuwa mlezi
wetu anatusaidia ada na michango midogo midogo. Ndo tumekuja kumshukuru. Ila
kama kaondoka Mungu ambariki huko aliko. Nikatumia siasa si ndogooo. Father
akasema kuna email yake naweza wapatia, akatuandikia kwenye karatasi,
nikakichukua mie. Sasa enzi hizo email zilikuwa mashikolo mageni. Basi haikuwa
riziki, tukaagana na shosti, sema kama hakuwa na raha flani hivi.
9 Have I not
commanded you? Be strong and courageous. Do not be terrified; do not be
discouraged, for the LORD your God will be with you wherever you go."
2007 akiwa A level, form 5 maisha
home kwao yakachange vibaya mnooo. Baba akaondoka kawatelekeza, mama hafanyi
kazi yoyote. Kiwanda kikawa kimefungwa, na hapo mtaani watu wote tulikuwa
tunategemea uchumi wa Kiwanda, maana wazazi wetu wote wanafanya viwandani. Sasa
baba yao alivoona maisha magumu akasepa kawaaacha na maza bila msaada wowote.
Na ada za private akadataaa. Afanyaje? Ikawa karudishwa home, za gvt ndo
hakureport, yupo yupo. Kanisa kaliacha anaranda randa tu mtaani. Ndo kunifata
kuniomba ushauri. Nikamwambia shoga unahitaji pesa uende shule, sio ushauri.
Bora mie nilifukuzwa fukuzwa private maza akachoka akasema wewe kareport tu
Kayumba nikawa nipo Kayumba tayari. Nani atakupa mamilioni uende shule kibwege?
Nikaikumbuka il email.
Nikamwambia ujue ile meail ninayo, tumcheki Fratery, anaweza kukusaidia hata
usome seminary zao bure, ama vovoe vile, hatokosa msaada. Kimbembe karatasi iko
wapi? Tukazama chumani pekenyua pekenyua matabu yooote ya Olevel mpaka
tukaipata. Tukaenda internent cafe, tukamtumia email wenyewe. Ikaendaaa. Wiki
nizma natoa 500 tunaenda kucheki kama kajibu holaaaa. Mi nikaishia hostel. Siku
hio nacheki ikawa kajibu. "Niko Parokia flani hapa hapa DSM, njoo tuongee,
nakukumbuka. imesainiwa Father ............................. Nikarudi home
ilikuwa Jumanne. Maza kanimind, we husomi, umefata nini, nikajitia naumwa naota
wafu, nikamtishaaa. Akaniambia kaa nimuite muombeaji wasije kukufanya ufeli.
Nikampasha shoga kiujumbe cha email. Nikampang ili asikilizwe aende mwenyeweeee
kama alivoambiwa. Nikarudi shule.
Akaja kuniambia nimsindikize,
anaogopa kwenda mwenyewe, siku zimepitaaa, huenda kamsahau, au vipi vipi,
akienda na mie hata iweje sitokosa maarifa ya kufanya hata ikitokea katutimua.
Nikamwambia sawa. Nikamwambia sahivi sisi watu wazima, mpaka nido zimelala
haitopendeza kwenda kumuulizia Father jumamosi ofisini. Mmmmmh! Twende kwenye
misa ya 3 afu tufanye manuvaa juu chini mpaka tumuone. Tukibahatika anaweza
kuwa yumo misani.
Tumeenda tumejiparaaaa, mimi
sijui hata kwanini nilivunja kabati siku hio. Shoga angu yupo juu ya mawe
lakini hela ya kusuka yebo alipata siku hio. Tumeingia kama watu vile kwenye
ibada. Ile mafather kuingia shoga akastukaaa. Sasa walikuwa mafther 3 wanasoma
hio misaaa. Mmmoja mzee, nikajua tu hawezi kuwa kile kizee, kwanza kiswahili
anajua Fresh, wengine wawili, mmoja ni mcute balaaaaaaaa! Looooh! Padri mrefu,
ana body flani amazingi afu HB ni hatariii. Mmmmh nikasema mbona majaribu tena.
Narudi kanisaniii kuimba kwaya kama mafather wako hivi. Hatari hiii. Nikawa
naomba Mungu tu asiwe yule tu yule HB ndo fratery. Mwingine wakawaida tu, kazi
ya upadri inamfaa kabisaaa. Mda wa komunio nikafanya maarifa mpaka nikaenda
kupokea kwa Lepadiri, mwenzangu hakwenda. Nikatamani nimuulize ni yupi kati
kati ya misa. Ikashindikana.
Misa kuisha, mwenzangu akawa
jasho linamtokaa, anasema twende tu nyumbani nimeghairiii. Namuuliza umeghairi
vipi tushafika hapa. Aaaah, nimeghairi tu, kama Mungu kapanga nisome nitasoma
tu. Hiii. Akapita mtu ananijua akaniuliza Lara unakaa huku na wewe? Nikamwambia
hamna tumekuja kumuona ndugu yetu Father mara moja tukaona tusali huku.
Akanitania isje kuwa Father flani tu akataja jina la mwisho, roho yetu kanisa
hili. Oooooh! Tutatona roho. Nikamwambia kama ni yule alietumikia bila kuongea,
yul mzuri unampa undugu na mimi unataka kuninyima nini? Yule hawezi kuwa ndugu
yangu miaka 800000 tena usinilazimishe. Hahahahaaa! Tukacheka. Akaniambia Lara
tutaonana wabayaa, huwezi kuja hapa mtaani kwetu kuchukua mali zetu wenyewe
tumekaa tu hapa. Nikamwambia ujanja kupata sio kuwhi, mie yule nikimpata
nitampa mambo ya hatariiiii. Hahahaaa! Tutakwa tunacheka.
Ghafla tukasikia Tumsifu yesu
kristu J! Tumsifu Yesu kristu na sisi, afu mtu kiswahili hajui vizuri. Mmmmmmh!
Sasa alikuwa nyuma yetu, nikageuka fastaaa na huyu shoga angu niliemkuta huku.
J ndo alikuwa kamface.
Nikageuka fastaa. Huyu hapa
Lepadriii, mmmmh! Tukajikausha kausha pale. Daaaah, roho iliniuma kinoma nomaa
maana ndo yule mcute. Basi ndo kumuuliza J za siku, J anampa hongera pale la
daraja la upadrisho. Mi namkata jicho shosti huyu mwingine ondokaaa na wewe, na
yeye kakomaaa. Kashajua pale kuna ishu. Le padri sio mmbongo za siku zipi?
Kajikausha pale pale. Tukaenda kunywa chai kwa mafather kule kama kawaid,
Burger, Cake, Cookies, baccon, cornflakes, Juice wanakula wale ni
balaaaaa. Shoga ananinongoneza Lara chama kubwa sikuweziiiiiiii. Kubwa la
maadui. Badae nikatumia inteljensia kumwambia yule kinganganizi nisindikize
chooni. Yule J nae asivo na akili nae anataka kuja, nikamblast sasa, kaa
hapo utusubiri, keep Reveland Fr. company. Akawa kama kashikwa ugoni han amani.
Chooni shoga ananiharakisha fanya turudi, nikamwambia tulia hapo, kwanza
nimeshikwa tumbo la kuhara. Chooni nafanya mmmmh! kumbe nipo nachat na Nokia ya
macho ya panzi. Shoga anahaha kama anaoga nje, fanya turudi. Kumbe mi
nimewapa chansi waongeee yao ya kikubwaaaa huko chooni. Nimetoka kunawa mikono
dakika 10. Kupaka make up dakika 10. Uongo mbaya chooni tulikaa zaid ya dakika
45. Kurudi kule shwariii.
Badae tukaondoka, shoga huyu wa
kumuokota njiani kamuomba Rev. Fr number, akampa TTCL. Hahahaaaa! Njiani
nikamuuliza vipi? Ulimwambia? Akasema ndio, kanipa namba hii, ilikuwa ya Voda,
kasema nimpigie kuna shule ya shirika moja Moshi atanifanyia mpango ada sio
kubwa na kuna mpango wa kuwasaidia Yatima na watu kama mimi kupata ufadhili
maadam Olvel nina Division 1. Nikamwambia basi poa.
31 but those who
hope in the LORD will renew their strength. They will soar on wings like
eagles; they will run and not grow weary, they will walk and not be faint.
Mi nikawa nakaribia Necta, so
sikufatilia sanaaa ishu zilienda vipi. Siku Necta imeisha narudi home, maza
ananiambia shoga ako J, anasoma Moshi una taarifa? Kapata mfadhili mama yake
kanisimulia, huyo mfadhili ulimtafutie wewe! Tobaaaaa, tobaaaa! Mmmmh! Nikaguna
guna pale sieleweki. Embu niambie mwanangu ulimpataje huyo mfadhili. Mmmmmh!
Nazuga, mama bwana ndo nini cha kushukuru anasoma baaas. Mtafutie basi flani,
na flani basi wafadhili si unaona wana lost tu hapa home. Mtumeeeee! Nikamwmbia
nitafanyia kazi hilo swala mara moja kusudi tu aniache. Nikasema J mshenzi
kweli, hata kuni update.
Sasa nikapata safari ya Moshi kwa
kaka yangu anafundisha KCMC, wifi alikuwa kajifungua hana msaada. Nikawa
nimeagizwa na bi mkubwa nikamsaidie badala yake walau mwezi. Kufika kule siku
wifi haendi darasani, nikamzukia shuleni kwao. Nikamsoundisha matron pale, akamleta.
Ndo kufurahi, nikaanza kumchamba wima wima ndo nini kuondoka vile? Akanipa
story kule simu haziruhusiwiiii kabisaaa. Siku anaondoka alimwambia maza anipe
anuani ya pale home awe ananitumia barua. Mambo gani ya barua. Nikamwambia tu
shoga pale home hamna muenda Posta, labda mdingi akiwakumbuka watu wake wa
Ulaya enzi hizo.
Ndo kuniambia shule fresh,
kalipiwa ada, na hela ya matumizi anapewa kaambiwa na Rev. Fr. kuna mfadhili
ila hakumtajia ni nani. Nikamuuliza vipi neno bado unasomaaa na kwaya unaimba?
Akasema hamnaaaa, ashakuwa mtu mzima. Nikamuuliza na kile chama chako cha
kutokunywa pombe bado upo? Akasema aaah wapi, ila sinywi. Nikamuuliza sasa siku
hizi unadate na nani? Naona vijana HB kabisaaaa, basi tu under age. Akawa
anajibaraguza tu pale. Nikamwambia to think of it sijawahi sikia una date mtu,
au ndo bado unataka kwenda kuwa Sister? Akasemaa hamnaaaa! Nasoma kwanza.
Mmmmmmhhhh! Nikamzuga zuga pale nikaishia. Nikamcheki mara moja church jpili.
Sasa jpili akaniambia kuna Ubuyuuu wa mtoooo. Nikasema niunguzeeeemie mpaka
nibabukeee. Ubuyu wenyewe Le Padri alikujaa. Alikuwa anaenda A town,yeye
alikuwa class, akaitwa na Brooder kuna mgeni wake.
Basi waliongea briefly tu,
akamuuliza masomo vipi? na general talk, if kama anahitaji kitu or anything
akasema hapana. Basi Fr akamwambia anaenda Italy atakaa 2 yrs maybe, so
hawatoonana, bt asome, na aendelee kumpotia matokeo yake kwa email, maybe post
card. Akampa na hela kwenye bahasha kubwa. Atumie vizuriii, manake yeye atakuwa
mbali kutuma hela itakuwa ishu. Akamuaga akaondoka na ma Fr. wenzie yeye kurudi
Hostel akauta $$$$$$$$$$$$ kibao kwenye ile bahasha. Nikamuuliza sh. ngapi
akasema nyingi. Nijue tu nyingi. Akanigea $200 za kula njiani nikirudi Dar.
Mmmmmh! Balaaaaa! Nilinunua nguo ni hatariii. Nikamfata tena jpili inayofuata
kumwambia hela hizo maybe za ada usizichezee wala usimpe mzazi wako, weka
akiba. Fungua ACCOUNT. Akasema hilo la msingi.
Basi ikawa likizo full kujiachia,
hela zipooo. Chuo nikikwama namtumia ujumbe wifi anamfikishia kanisani naletewa
$200. Badae akaniambia hakuwahi kudaiwa ada wala sh. 100 shule, ile hela ikawa
yetu ya kutumia. Kwa raha zetuuu.
Alivomaliza 6, nikamwambia acha
mambo ya kanisaaa, nampa pointer jinsi ya kuvaaaaa kimjini, pesa si anayo,
tunaenda out sehemu za maana, tuna roll big. Akawa tunaishi wote Hall 4 likizo
yote ya form 6.
Ikawa wakaka wanamuelew sasa
mapigo yake, afu ni mzuri sanaa tu kwa asilia. Akawa kila mkaka anamtoa kasoro.
Kila mkaka anamtoa kasoro. Nikamwambia utazeeka, ukiendelea na hio attitude ya
feeling too good for every man. Ikawa anadate lakini ndo hivo mapenzi ya bongo
sanaa nyingi. I am sure alivoanza nae UD mi nikawa 3rd year tunaishi Hall 4
wote, alinunua yeye room nzimaaa. Alivofaulu na 1 ya hatari, Rev Fr. alituma
tena Euro za kutoshaaaaaa. Cluba gani hatukuingiaaaa? kiwanja gani
hatukufika? Mpaka Zanzibar. akiwa mwaka wa pili mimi nikawa nishamaliza
niko kitaa sasa, ananitoa tu kishkaji mpaka nikaanza kazi na business yangu ya
kuuza wake za watu.
Sasa akiwa second year, Rev. Fr akamwambia
anarudi April hapa Tz. Akifika atamtafuta. They have so many things to catch
up. Mmmmh! Siku hio kanipigia come, come, Rev. yupo town he wants to meet for
dinner. I have to look good, i cant get this wrong, it is important uwepo, nime
panic. Njoo tushauriane. Nikamwambia kwa $$$ na Euro nilizokula za Rev,
najaaaaa. Nikitoka kazini tu nipo hapo Hall 4. Hahahahahaaaaa!
13 No temptation has seized
you except what is common to man. And God is faithful; he will not let you be
tempted beyond what you can bear. But when you are tempted, he will also
provide a way out so that you can stand up under it.
Basi kufika nikamkuta shoga wa
mie katoa nguo kabati zima haoni ya kuvaaa! Tobaaaa! Nikamchagulia pale gauni
decent tu yet chick. Yuko this is too holly! Nikamwambia mmmh, you are
meeting a man of God, you have to look decent with him. Hata kama you are
meeting for Dinner in a hotel ila yule lazima aj na ile mi collar yao, people
will know he is priest, dont go like like a hooker,it will make him
uncomfortable. Akasema okay basi nava hizi. Nikamwambia those are too cheap!
Vaa hii gauni tuliinunua kwa yule dada wa nguo za UK, it is a brand, it is decent
n chick, plus it screams money and class. All the money akikuta you still look
cheap atakudharau. Mmmmh! Akakubali kishingo upande. Sema chini akatupia hills
moja Zara ya hatariii, na handbag matata. Alipendezaaaa mnooo. Nikawambia
chondechonde naomba live broadcast ya hio dinner what up. Hata pastor akienda
chooni nijulishweeee. Atachosema nukuu. Min nitakuwa home ila nafatilia live
dinner home.
Whatsup ikaingia hiooo.
Rev.kanisifia ni hatariii, anadai i have grown to a beautiful lady he never
imagined. He likes me like this all classy, educated, it is better
alivonisaidia i deserve this life. Mmmmh! Akamwambia tu Italy was boring,
anapenda Tz kuliko sehemu zote alizokaaa.
Then akani whats up, Rev kaishiwa
story, yupo tu kimyaa. Nikamwambia nenda chooni kwnza aione shepu hio vizuri,
ukirudi inama kufunga kiatu kichokozi hakikisha anakuona. Hahahaaaa! Kanimabia
nimerudi chooni hapa ni balaa. Kadataaaa! Nikamwambia imetosha we muage,
mshukuru sana sanaaa sanaaa, sanaaaa kupitiliza kwa wema wake wa zamani,
mwambie you owe your life to him, anytime he need to talk or ANYTHING he can
tell you, asisite. Moyoni mwako yupo level zingine. Ile kumpa invitation to
treat ya codes. Husemi direct. Afu muage ondoka.
Rev kamrudisha mpaka Hostel.
Anani update hapo. Nikamwambia mtext you liked his company so much, you wouldnt
mind meeting again. Akamtumia. Rev akamwambia poaaaaa! Will definately meeet
soon.
Romans 13:8 Owe no one
anything, except to love each other, for the one who loves another has
fulfilled the law. I
kawa wana chat chat na Rev. na
nini. Ila meting ya pili ilikuwa bado. Akaniita njoo ulale huku hostel. Sasa
mda huo nilikuwa na kibwana kisumbufu hatari. Kina wivu ni balaaaaa.
Nikamwambia mi kesho naendakulala hostel so ukitoka kazini usinifate kazini.
Ooooh unaenda kwa vibwana sijui nini.
Mie huyo hostel. Usiku mda wa
kulala ndo kunipa ubuyu sasa. Ooooh Lara wewe ndo msiri wangu, sahivi wewe mtu
mzima, najua utanijudge but inabidi nikwmbie manake ushoga kazi. Wewe hii ishu
ya father unaijua nje, ndani, sasa nataka unishauri kitu maana nataka kufanya,
inshort nishafanya maamuzi ya kipumbavu, i just need one person, just 1 person
to tell me she understands and i will go ahead. Inaeza kuonekana
ufalaa mtupu but that what the real me wants, and i have to do it, i just have.
Nikamwambia cut the bull shit,
shoot! I want to DATE THE PRIEST! Shampeni ilinipalia ghaflaaa! Actually i knew
she had the hots for him all allong but hearing it comming out of her mouth was
another thing! Different level! Paliwa tu upaliwavyo ila ukweli ndo huo. I
always wanted him. Ata first i didnt know what was it but now i am sure,and i
am not ashamed.
Sasa sijakuita hapa for Moral
talk, spare me the sentiments ningetaka moral tlk will have spoken to my mom!
Hahahahaa! Nimekuita hapa unisaidie how can i make it happen? How we can make
it happen? Tulikula wote hela zile. Tobaaaaa!
Nikamuuliza tu WHY? ndo
lililonitoka. WHY? Unamuuliza nani? BECAUSE! Akaniambia sikia,think about it,
nimedate na watu kadhaa, ila hatujawezana cause they dont care. Yeah! Usanii
mwingi, bt Rev.alinisaidia when no body was there for me, hata leo atanisaidia
nikimuomba na haombi kitu. WHO DOESNT ASK FOR ANYTHING DESERVES EVERYTHING!
Dont you thi so! Nikamjibu Nope!
Not one bit. Akasema sikia, think of the money i will get when i amwith him,
and you will still be friends with me to spend it! Well she kinda of spoke my
language.
Nikamwambia mimi nitakusaidia but
lets be direct. Nakusaidia sababu ya umalaya wako tu, na tamaa zako za fisi
umemuelewa mtumishi, in return i get financial favors. Kujifanya unataka
utembee na mtuishi kila alikusaidia huo ni uongo na kuufanya msaada wake wa
mwanzo kwetu kuwa UNPURE. Kitu ambacho si kizuri. Akajibu whatever you want to
think of it, if it will make you sleep at night lets get to action.
Nikamwambia maybe he likes you
too! Kumbuka alikwambia come alone at that age? Anhaaaaaaaaaaaaaa! Mmmmmhhhh!
Nendasecond date tumsikilizie, he might start the fire works himself. Ila kaa
ukijua if an only if he asks once, go for it. He will never ever ask twice.
Nikamwambia ila shoga we malayaaaa! Mpaka madhabahuni umefika ni shidaaaa!
Hahahahaa! Tukacheka tu.
Exodus
20:14 - Thou shalt not commit adultery. Matthew
5:28 - But I say unto you, That whosoever looketh on a woman to lust
after her hath committed adultery with her already in his heart.
Basi ikawa Rev. Fr hasemi
meeting lini. Shoga akawa obsessed na Rev. akaacha kabisa ku date watu
wengine. Ananiuliza mbona hasemi lini hio meeting bwana. Nikamwambia sikia IT
IS NOT EASY FOR HIM TOO. Mwenzio ana kiapo cha milele, ukiona anakukwepa ujue
hajiamini what he will do next. And for him kuzini ni ngumu sanaa, imagine
umezini afu unapanda madhabahuni ale kuhubiri watu wazini kwenye madhabahu
takaifu ya Mungu, mbele za Mungu mwenyewe. Inataka moyo. Akikasirika utashangaa
ngumi inatoka juu inamtandika. Hahahaaaaa! Tukacheka. Nikamwambia for him to
sin it has to be really worth it. Na isitoshe anaogopa maybe you are not in the
same page. Akutokee, umkatae uende kwa paroko, gazetini, sio boya kiasi hiko.
Act mature huyu Fr. wetu mbonaaa.
As unplanned second meeting ikawa
Parish kwao huko kulikuwa na Jubilee. Sasa mandhari ikawa sio sio kabisaaa, and
she barely saw him. Akarudi disapointed kichizi. Akaniambia mtumishi anaenda
Arusha kamuaga. Nikamtania kama mimi ndo wewe, namlegezea sauti mumishi naomba
lift, i need to go to A town. Tukifika yeye atalalaa jimboni nachukua
Hoteli town pale, namwambia niko hotel flani, you can come say Hi! Hahahahaaa!
Akija hachomoki. Even the devil himself cant resist this plan. Najipeleka ready
to ship status mwenyeweeee. Hahahaaa! Akija najifanya nimelewaaa.
Akaniambia wewe ujue huna akili
kabisaa. Hahahaaa! Asipokuja hotelini utafanya vipi? Nikamjibu natengeneza
tukio, namwambia mdada wa mapokezi ampigie naumwa, afu nimelewa, like nimepata
bad news, akija tu mule ndani namdaka na mibusu moto moto, japo yeye ni Fr. ila
mwanaume vile vile lazima aonesha ushirikiano. Silaha ya shetani siku zote iko
kwenye uanzilishi. Najifanya sijielewi namuhug hug si unanijua mimi nikiwa
location? Hahahaaa!
Akaniambia toa uchizi wako hapa.
Nikamwambia wewe kaaa hivo hivo usubiri fate ichukue mkondo wake. Wenzio
wanafunga na kuomba ma Fr. waepushwe na watu kama wewe. Nikamwambi
nakutania mwaya Dont be so cheap! If it is meant to be, it will be.
Siku hio ya alamisi akanitext
niko njiani naenda A town na Rev. Fr. Tobaaaa! Nikamtext you are not going
along with my plan are you? Akasema EVERY PART from plan A to B. Nikasema
mazafantaaaaa! Nikamtext acha usengery usiku Fr. hayupo huko tulipo. Inaweza
ikawa mtu wa Mungu kweli ukawa umemkosea adabu kupita mipaka, akaublock
kwenye simu, na kujilaumu kumsaidia changu. Abor the mission. You never know
till you know. Kutaka kula nyingi utajikuta umeliwa KINGI.
Akanijibu maneno yangu
mwenyeweee, "Japokuwa Fr ndio ila mwanaumee" we never know till we
will know! Hapa niko njiani too late. " Daaaah! nikawa moj haikai, mbili
haisimani. Nikashikwa mpaka na tumbo la kuharisha.
Akanitext jioni Fr. is on the
track, anaenda kulala jimboni but kanishauri nichukue Hotel hapa Impala. We are
on, kaa standby kwa paln C and D. Nikamjibu sababu sikukupa go ahead nazima
simu, utajijuaaaa. You are on your own. Nikazima simu.
Nikawasha kesho yake, akanipigia,
Fr. atakuja leo kunisalimia, na mimi naona nianze na plan B. Tobaaaaa! Hapa
nakunywa wine toka nimeamka. Nikawa sina raha kabisaaaa. Nikazima simu
niconcentrate na kazi. Usiku saa 5 nikaiwasha kimachale machale
akanipigia.
Huwezi amini, nimefanya ile plan,
ime Nokiiii! Nikasema WTF! Tushahairbu. Maana hii ndo ile mechi kosa la defence
bao. Akaniambi tu, nimejiongezaaa nimejiongezaaa holaaaa! Mpaka nimemkumbatia
akaniambia you have had too much to drink, akaondoka. Aliongea kistarabu
lakini sio kuni blast au vepe.
Mmmmmh! Nikamwambia he will be
back tomorrow morning usitoke humo ndani. Kauli mbiu yetu Japo Fr. ila na yeye
mwanaume vile vile. Tukachekaaaa. Dont deapair be ready. Akija kesho mikao ya
kihasara hasara kama kawaida. Tena umuangalie machoni, akijiloga kukuliza abt
ishu ya jana be direct, nakutakaaa. Kwani kitu gani? Be confident hata usiyumbe
yumbe. Hapa tushafika point of no return.
Saa 9 akanitext you were right,
kajaaa! nimempa basha sha helllo Fr. kama hamna kilichotokea janaaa,
utaniwezaaa? Nikamwambia sikuwezi shoga angu usisahau kumuangalia machoni.
Akaniambia shoga sikukupa ubu huku anakuja na mikoti pull neck collar
haionekani. Tobaaaa! Nikamwambia huyo yupo ready to ship kabisaa
Basi ikawa kimyaaa mpaka kesho
saa 4. SMS hazijibiwi, simu hazipokelwei. Nikasema HAPA TAYARIIIII! Ila
nikawanataka tu ule uhakikaaa na DETAILS, Baby details! Mtumishi yule, nikawa
nataka A to Z.
Luke 15:21 Father, I have
sinned against heaven and against you. Psalm 41:4 O LORD, have mercy on me;
heal me, for I have sinned against you."
Akanipigia kesho saa 5, ndo
kaondoka sasa hivi hapa, acha tu. Niamkatiza, kabla yayote TAYARI au BADO?
Akaniambia tuliaaaaa, nakupa mkanda mzimaa, A to Z, siruki wala sipeleki mbele,
mstari kwa mstari.
Nikawa naona kama napaa sasa.
Nikamwambia leta picha hilo. Akaniambia kaja hapa, kama kawaida nikajifanya im
not ashamed, inshort toka safarini ilikuwa nishamzoea so hakunipa shida wala
nini. Basi nikaw namchekea chekea hivooo. Tukala, akajiloga akapita mule mule
kuniambia jana you had too much to drink, na English yake ya Kizulu.
Na mimi nikatumia falsafa, kufosi
KINGI. Nikamwambia tu, alcohol brings out the inner us, it gives us balls to
say what we cant say when sobber because of many reasons. Lepadri akawa
ananiangali machoni lakini ile romantic sasa, na mie nikawa nimekazia jicho la
kulegea, ila nafsi zinaongea. Kweli macho ndo mlango wa roho.
Tofauti na nilivotegemea ataona
aibu, akaleta ligi nae ya kifalsafa na theolojia nae. Usije kuzani mwepesi,
mzitooo hatari. Akaniambia so what are you telling me? Kwa tabasamu lile la
kifirauni wanaume wanalotoa. Sneaky and sexy at the same time. Nikamjibu i am
telling what you want to understand, wewe mtu mzima. Mmmmh! Fr. akaguna. So you
were not drunk? And you understand i am a priest right? Aauliza Fr. Akamjibu
200% Yap!
Father akaendelea na mdahalo wa
maswali na majibu. Akamtwanga lingine! "And you are still interested to
explore other unavailable options?" Akamjibu "Forgive me father
for i am about to sin"
Padri akawa anazidi kudataaa,
lakini hajakubali kirahisi.
Akamtwanga liningine."You
know i am a man of God right? Then WHY me? Why not other men? What is in it for
you? You are damn beautiful, you can have any man you want?
Akamjibu tu, BECAUSE I DONT KNOW.
I just like you. Maybe because you were so nice to me at my darkest moments. Or
because it is you. All i know is i am into you, at first i had mixed feelings,
didnt understand it, but now im older, matured, wiser, and i know what i want I
know you are a man of God like li know my own name, but you still a man, a good
man, better than the rest i met, and i am woman, i feel things, things i cant
explain." Hapo anakwambia kamlegezea jichooo zaidi ya Delila kwa Samson na
zaidi Jezzebel, zaidi ya Rahabu kazini. Ooooooh! Father kiti hakimtoshiiii,
akwa sasa yupo comfused.
Akatwanga swali."But you
know i am a man of God and i wil not leave God to become anything, or live any
other way.There should be no exceptions. No hope, no future. J Akamfanyia shhhhhhhhhhhhhh!
Hapo akampa mabusu moto moto, wakaingia ulingoniiiii. Collar ikatundikwa juu ya
hanger. Haariii.
Ananiambia sikutaka kufanya
makosa, nilimpa mamboooo, nilimpa mambooo acha kabisa. Ukizingatia mwenyewe
nilikuwa na kiu cha miaka. Acha tu. Nimeshka MIC, haijandoka hata mojaaa,
zote nimezimezaaa. Yaani nilitaka kumuachia impression ya hatari. Kalia kama
mtoto mziki wangu ulivokuwa mnene CD 700.
Mmmmmh! Nikagunaaa. Nikamuuliza
zana ilitumika? Kinga? Yupo bwana tumekanyagia ringi! Acha tu. Nikamuuliza sasa
ukipata mimba si balaa. Akaniambia acha tu ila jua zana haikutumika wala nini.
Mmmmh Makubwa! Hapaimewasha AC mpaka mwisho. Ni balaaa. Kiuno spring zote
zimeachia. Hahahaaa
Romans 3:23 For
everyone has sinned; we all fall short of God’s glorious standard.
Ikawa hakwenda tena pale h8telini
ama kumtafuta. Akaniuliza nimtafute, nikamwambiaotezea we rudi chuo.
Akikutafuta poa, asipokutafuta poa. Akwa kapanda Dar express anarudi Dar. Rev.
huyu hapaaa, kamtext. Kimya sanaa. Akamwambia yah, im going back to Dar niko
kwenye Dar Express. Akamwambia shuka Chalinze nisubiri na mimi ndo natoka huku,
nitachelewa.
Kafika Chalinze kachukua lodge
kakaaa, usiku Rev. huyu hapa. Mechi mpaka asubuhi. Ila kila mtu akaondoka
kivyake. Sasa ikawa Faza kadata ila bado hajadata vizuri ile ile kuwekewa Dupli
kunene. Kufika mjini Rev. akamwambia inabidi uhame hostel, i need to spend more
quality time with you. Tafuta nyumba nzimaaaa, iwe uzunguni, kumetulia kuna
privacy, nitakuwa nakuja kwa mda wangu.
Basi tukatafuta ya kwanza Sinza,
akaikataaa iko uswahilini, ya pili mbezi beach akaikataa pia. Tukawa bado
tunatafuta ingine. Siku hio hana ili wala lile 1m ikaingia kwenye simu, na
kesho 1m tenaa za matumizi tuuuh. Hatariiiiiii. Danger! Ikawa nyumba bado
kupatikana.
Akamuita Upanga siku hio kwenye
appartments moja kali balaaa. Wahindi tu na wazungu. Wakashinda pale, wakafanya
yao. Usiku Rev akaondoka kwake Parish. Akamwambia usiondoke kesho nakuja.
Usiku kaniita nione hio sehemu ilivo baddest. Mi roho iliniuma sanaa hawa watu
wanavoishi kama ulaya. Mmmmmh! Nikasema ikitokea Askofu kakosea njia
najilengesha kama mambo ndo hivi balaaaa. Asubuhi nikaondokaa.
Ndo kumwambia ile apartment ni
yake, akae tu pale, so that they can spend more time together, ila it comes
with conditions. Hakuna kuleta mtu wa aina yoyote mule iwe wa kike au wa kiume
au ndugu. Ni yeye tu ndo awe anaishi pale, then Rev atakuwa anakuja kwa mda
wake, kila mtu na funguo yake. Mmmmmh!
Nikamwambia shoga kubaliiii! Tena
kula na kipofu, usimbane Rev kabisaa, endesha mambo kiutu uzima, usimbane
kabisaaa. Mood, attitude usiendekeze kabisaaa, wala usimfanyie kiburi na nyodo.
Hivo mwikoooo! Kabisaaaa! Wewe yule unamuheshimu kama baba yako mzazi, kila
kitu kwako sawa tu. Atakutoa kimaishaaa.
Ikawa bibie ndo anaishi pale.
Sasa pale ndani mule hazikosi m2 au 3 zipo tu za kuchukua kutumia. Mda
mwingiine Rev anakaa wiki 2 hajaonekana. Anaanza kupanic namwambia ngoja upate
free p mko wote masaa 24 hamna mbele wa nyuma, vumilia mbona jambo dogo sanaa
hiloo. Akirudi usimuulizie alikuwa wapi wala nini, malovee tu.
Rev. Mwenyewe akakubali kwa
kinywa chake laiti asingekuwa padri angemuoa. Ila ndo basi tenaa ishakuwa
hivooo. Akashangaa watu ndoa zinawashinda wakati peace of cake kwake mwenye
double life. Hahhaaaaa! Ikawa ndo hivo. Anaishi pale anajiachia kabisaaaa.
Siku kanipigia simu Lara 1,
naomba uje now now. Nikamwambia bwana weee Fr. Akinikuta huko itakuwaje. We
njoo tu. Njoo na vipimo vi 5 vya mimbaaa! Tobaaaaaaaa! Nikamwambia nakuja.
Nikasema moyoni TAYARIIII HUKO.
Proverbs 28:13 People
who conceal their sins will not prosper, but if they confess and turn from
them, they will receive mercy.
Kufika kule kojole vipimo vi 5
vyote positive. Tobaaaaaaaaaaaa! Tumeeeeeeeee! Akaniambia hapa la kufanya mpigi
P, twende kwa Dr wake. Si alishusha juzi juzi tu? Mmmmmmh! Nikamwambia
ila mtaarifu Mtumishi, sio jambo la kuamua peke yako.
Akaniambia Lara unakuwa kama
falaaaa, nimwambie nini sasa, we si unajua kanisa linavokataza haya mambo,
atanielewaje, bora nifanye nimwambie nishafanyaaa. Ataniona kidogo niko
responsible for my mistakes. Nikamwambia tulia kwanzaaa. Kapanic nitulie nini
utaka ifike miezi mi 5? Mmmmmh! Nikamwambia we tulia tukapime hospitali. Tupate
uhakika. Twende sasa hivi. Kitu pwaniiii. Miezi 2. Tobaaaaaa!
Ikawa hospital kuna vitoto
vingiii, akwa anaviangalia, akawa anajimbia of all men in this life time, toka
moyoni mwangu napenda kumzalia Rev, basi tu our fate is cruel. Mi nimeshikilia
maamuzi yangu we mwambie tu, tumuone reaction yake, kama mbaya utatoa tu, kuna
o.oooo1 chance mambo yakawa mazuri huweziii jua.
Mmmmmh! Akasema nitajaribu
kumwambia nione itakuwajeee. Ila kikinuka ujue ni wewe na makosa yako.
Nikaamwambia huwezi jua. Basi jioni hio kurudi kamkuta kesharudi. Ufyoro
tulioufanya wakati tunakurupuka kwenda hospital vile vipimo hatukuvitupa nje,
tuliviacha vimetapkaa chooni.
Kuingia kakuta kaviweka juu ya
kitanda, vyote 6. Afu kakaaa kitandani. Ananisimulia akajikuta tu kaanza kulia
kilio cha mtu mzima, sauti haitoki machozi tu. Tofauti alivohisi huenda Rev
atanuna au vipi, kumkasirikia, akaja tu kumu hug, akamwambia it is okay.
Usikose raha, we will solve this. We are in it together. I am with you all the
way.
Akamtest haina shida mi nitatoa.
Alistukaaa Rev. usiongee tena kitu cha kipimbavuuu kama hiko. Umuue mwanangu,
damu yangu. Au ushatoa zingine bila kuniambia? Kabadilika kabisaaa. Akajitetea
hamnaaa, i just thought i would do you a favor. Akamtatisha na kumblast, when
did i ask you to do me any favors? Basi ikawa kama kajistukia he was harsh!
Akamuhug tu wakanyamaza mdaa. Ndo baadae akamwambia hakuna kutoa hii mimba, it
is a gift from God, we keep it, BUT IS SHOULD NOT HAPPEN AGAIN. Be extremly
careful!
Ikawa kaambiwa aende regency,
akaletewa na gari ya kutembelea. Fr. anapiga simu mara 5 kwa siku,
unajisikiaje, umekula, unakula nini leo, anasemaje mwenzio. Yaani macate ndo
yakazidiii ni balaaa. Kila baada ya siku 2 anakuja. Akampeleka mpaka S.A kwao
kabisaa akamuonesha tu kwa ndugu zake pale, hakumtambulisha tu. Bt akawa anamwambia
incase of anything make sure mwanangu anawajua ndugu zake. Sasa ikawa wamekuwa
kama ndugu sasa. Shopping ya maternity huko South ilikuwa balaaa.Hayo yote
ndani ya mwezi huo huo wa taarifa.
Kurudi huku siku akasikia tumbo
linamuuma hatari akaona bleed! kwenda regency Dr. Akamwambia mimba imetoka,
sema coz ni ndogo itaisha kwa bleed. Akawa karudi na Rev yupo. Akataka
kumwambia, Rev akawa kaja na file, kiwanja Salasala akawa anamwambia inabidi utunze
hii hati, im building for you and our baby, kuna leo na kesho, i want my baby
to grow in a nice home. Hakumwambia kama there is no baby anymore.
Akanipigia. Amwambie au auchune
na ujenzi ushaanza?
1 Corinthians 13:4-8 Love
is patient and kind; love does not envy or boast; it is not arrogant or rude.
It does not insist on its own way; it is not irritable or resentful; it does
not rejoice at wrongdoing, but rejoices with the truth. Love bears all things,
believes all things, hopes all things, endures all things. Love never ends. As
for prophecies, they will pass away; as for tongues, they will cease; as for
knowledge, it will pass away.
Nikawa nimekosa amani
kabisaaaa. Yaani moja haikai mbili haisimamiiii. Nikasema NO SWEAT, mwambie tu
ukweli. Who knows. Akasema akija tu leo namwambia Mimba imetokaaaa. Nikamtafuta
mchizi wangu akili kubwa P. Huyu dada ni kichwaaaa, straight A's lecturer
sahivi. Kama mnakumbukaaa ile story ya MR. POLICEMAN, ndo huyu sasa. Basi
nikamwambia ninunulie bia, na mawazo kichiziii.
Ndo kumsimulia sasa A to Z ya
hii movie. Nikamwambia imebidi tu amwambie ukweli. Akaniambia nyie
wasengery nini? Amwambie nini? Ili iweje? Acheni mambo ya kimaku, hamna
kumwambia lolote. Hapo dawa ni kutafuta mimba ingine kimya kimyaaa. Tena mimba
ikitoka mwanamke anakuwa fertile kinomaaa. Mwezi huu akikomaa inaingia upya,
mwakani mda kama huu tunalea wenyewe.
Ndo akili ikanirudi,
nikakurupukaa kumpigia kama bado hajasemaaa. Akawa hapokei, nikajua ndo yupo
nae hapo. Yule dada akapiga kwa namba yake, akapokea coz hakujua nani.
Akamwambia mi flani huo usengery aliokushauri Lara usiufanye, nyamaza kimyaaa,
iko njia ya win win. Akasema sawa mwalimu, kesho nitakusanya kazi. Kumzuga
pastor
Kesho akasema nipeni data
kamili. Akaambiwa hapo inatkiwa aende kwa expertufanyike utaratibu apatemimba
ingineeee, yani tunambabatiza Rev mchana kweupeee. Akawa kaenda sasa. Kweli
kufika kule akaambiw uwezakono upo, ila ghali sanaa. Mnanake inabidi
wacheze na hormones, mirija waikague, wizi mtupuuu. Akasema hela sio kesi.
Kama haitoshi akaenda na kwa
wataalamu wa katiba za mabibi. Ukitaka kuchangany jinsia kuna mti wake
unakunywa, ukitaka kubeba kuna mbegu unasagiwa, Ukitaka mapacha dawa pia iko.
Chango dawa iko. Zinatoka zisitoke dawa iko.
Tukaenda saa 10 usiku ushoga
kazi. Manake folleni lake kwa huyo mkunga sijui mwanga, sijui mganga ni ndefu
hatariii. Kuingia saa 7. Akamwambia imetoka, nataka ingine mwezi huu na safari
fanya maarifa isitoke.
Akamwangalia akamwambia lakini
afya yako sio nzuri. Inatakiwa ukae walau miezi mi 3 ndo ubebe tenaaa. Rudi
nyumbani hakuna msaada. Ningekusaidia ila itakudhuru mnoo unaweza hata ukafa.
Nakuona damu iko chini, afu asili yenu mna uzazi mgumuuu sanaaa, hiki
unachotakakukifanya kwa afya yako ni hatari sanaa. Nendeni tu, folleni ndefu
wanangu.
Mpambe nikaweka 100,000
mezani. Wakaangaliana mkunga na msaidizi wake. Mkunga akatafakari akasema kweli
nendeni ni hatari sanaa. Nikaweka laki ingine mezani zikawa 2. Ujue mi
mtoto wa kitaa najua hela inaongea kwa kelele kuliko maneno. Mkunga
akaenda uwani na msaidizi kujadiliana. Walivokuja nikawasoma fasta nikaona jibu
lao halieleweki kama wanakomaa na msimamo wao. Alivokaa tu, kabla hajaongea
nikaweka laki 2 tenaaa. Mkunga akamuangalia msaidizi wake, wakakubaliana
kitu kwa ishara. Akasema dawa ipo lakini ipo Bukoba ni ya kutengenezea ziwani
maana majani yake yanaota ziwani tu, na inabidi ichanganywe mabichi. Ina kazi
kubwa sanaa. Nilimtengeneza mwanangu na mkwe wangu ndo walikuwa na uzazi mgumu
kama wako. Rudi baada ya siku 3 kuna anakuja na ndege kesho, sitofungua siku
yote inyofata niitengeneze hio dawa. Na zingetoka nyingi sanaa. Ila hapa
halijawai kushindikana jambo.
Akawa anawaza kweli yani.
Manake mkunga nae hakuwa na habari njema wala nini. Ikawa kamameli
inazama. Siku ya 3 ikachukuliwa hio dawa, akainywa. Akawa kazi moja kumhada Rev
atoe penzi mfululizo mimba ipatikane tenaaa. Akawa anajifanya kuumwa, mara yuko
horny ilimradi tu game ipigwe. Kila baada ya wiki anakojolea kipimo. Holaaaa!
Wiki ya pili Holaaaaa!
Wiki ya 3 kitu pwani. Basi
ikawa sasa sio kama ya kwanza, inamsumbua hatariii. Anaumwa umwa balaa. Siku
katoka U.E ya mwisho kazimia huko chuo. Ndo badae Rev Dr. anamuelezea
huyu mimba ya kwanza ilitokaaa akamuangalia usoni J akaminyia jicho Dr. Basi
Dr. mwenyewe mwanaaa, akabadili CD katikati ya movie. Eeeeeh inatokeaga
complication, ni hali ya kawaida, sidhani kama alikuwa anajua. So inaonesha na
nyingine imeingia bila nyie kujua. Ni mtihani tu. Ila huyu mama anatakiwa
kupumzika sanaaa, na uangalizi wa karibu mnooo. Inaonekana mwili wake upo
fragile.
Weeee! Rev
alimsikitikiaaa, akamuonea hurumaaaaa. Basi ndo macare yakazidiiii. Uzuri
alikuwa ashamaliza chuo. Akawa anakaa tu anailea mimba. Mahaba ndo yakazidi.
Dr. ofcourse alipozwa na chochote kitu cha 500,000
Galatians 5:19-21When you
follow the desires of your sinful nature, the results are very clear: sexual
immorality, impurity, lustful pleasures, idolatry, sorcery, hostility,
quarreling, jealousy, outbursts of anger, selfish ambition, dissension,
division, envy, drunkenness, wild parties, and other sins like these. Let
me tell you again, as I have before, that anyone living that sort of life will
not inherit the Kingdom of God.
Ikawa Rev yupo bega kwa begaaaaa.
Anahudumia fresh vibayaaaa. Mjengoo unaendeleaaa. Akalea mimba kwa raha vibaya
mnoo. Ile unajisikia kula nini. Unataka nini, acha tuuuu. Alibokaribia kuzaa
akaenda kwao kujifunguaaa. Mungu mkubwa akajifungua kidumeeee. Kina afya
teleee. Padri alifurahiii siku hio. Akamfanyia transfer m 5.
Olaaaaaaaaaa! Kurudi kule kwake
nursery ya kufa mtu. Bwana weeeeee! Acheni tu. Kitoto chubby chubby. Padri
kapiga biti hakuna Hg wala nini, ni mwendo wa kulea mwenyeweee.
Kitoto kikawa kinapendwa na baba
yake Mpaka raha. Yani mtu mwenye raha utamjua tu. Anashinda ndani kwake
24/7.
Hakuna raha zisizo na mwishooo.
Siku hio Fr akamwambia mimi naumwaa. Naumwa sanaaaaa. It could be
cancer. But naenda kwa vipimo nje. Kaza roho. It could be just a bad wind
or it could be the end. Nakuachia hizi m. 15 uzitumie vizuri manake hujui na
mimi sijui nitakuja liniii. Naweza hata nisijeee.
Alilia siku hio. Kukawa na msiba
mpaka kwa mashosti. Fr. ndo hivo tenaaaa. Aliliaaa. Fr. Akaenda nje kwa vipimo.
Shoga huku maisha hayaelewi. Pale kodi ikawa imeisha kwenye appartment akataka
ahamie Salasala kwenye ghorofa. Tukamwambia pangisha nyumba hio upate hela ya
kula
Akarudi kwao na mtoto. Pesa ndo
hivo za kipimo. Akaenda na kutafuta kazi. Rev akipiga simu hawasikilizani! Rev.
Anamwambia mi naumwaaaa, niko critical ndo maana sijarudi. I dont have access
to money. Sijawahi kukunyima hela, ukiona sikupi ujue sinaaaaa. Bibie
ooih kama vipi waambie ndugu zako una mtoto wakusaidie kulea. Mi siwezi peke
yangu. Sijui nini.
Watu wakasema tumchambeee. Hawezi
kumfanyia mgonjwa vileee. Wengine wakasema tumuache tu, kichwa chake hakipo
vizuri, mambo mengi yametokea mda mfupi. Akitulia atajirudi. Manake ujane wa
usichana si mchezooo. Na mtoto yule ndo wa kudumuuu.
Basi akatafuta kazi uzuri
akapata, ndo na kupata hela akili zikamrudi. Ndo kuanza kureflect alivomfanyia
mgonjwa. Ikawa Fr. Kapiga simu ila hata anavoongea unamsikia tu hali si nzuri
kabisaaa. Basi ndo akamuomba msamaha na kumwambia sahivi anafanya kazi, ataweza
kumlea yule mtoto.
Ndo akamuuliza yupo hospitali
gani? Huko U.S. basi akawa anamwambia. Nafanyiwa chemo ila bado hali si nzuri.
Sidhani kama nina mda mrefuuu. Bibie akajichanga akaenda U.S na mtoto
kumpelekea walau amuone mara ya mwisho mwisho. Anakwambia hali aliyoikuta huko
si hali. Ana hali mbaya mnooo. Kabakia kama fuvu. Mmmmmh! Picha huangalii mara
2.
Ndo karudi sahivi, anahaha tu.
Hana hamu. Ndo kila siku kuwaza tu, sijui tayari sijui bado. Yani kesho haijui.
THE END!





